Shirika la Nyumba Zanzibar imeikodisha kampuni ya Mardev Limited yenye makaazi yake Morocco Nyumba zake nne, nyumba hizo zenye namba 288-289 ya Hurumzi, 291 ya Forodhani, 291B ya Forodhani pamoja na 292B ya Kiponda. Tukio hilo lilifanyika siku ya Jumatatu tarehe 07/06/2021 katika ofisi za Shirika la Nyumba Zanzibar.
Akiongea katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar, Mwanaisha Alli Said, alisema Nyumba hizo zimekodishwa kwa kampuni hiyo kwa ajili ya maakazi na wamepatiwa mkataba huo baada ya kufikia makubaliano yote pamoja na kuwalipa waliokuwa wapangaji wa nyumba hizo awali.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alisema mara tu baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo mpangaji huyo ataruhusika kutumia nyumba hizo. Pia aliwasisitiza Mardev Limited kuzitunza nyumba hizo pamoja na kufuata na kutii masharti ya mikataba hiyo
Mikataba hiyo ilisainiwa na Mkurugenzi Mkuu Bi Mwanaisha Alli na Shahidi wake Afisa Sheria Ndg. Taufik Bushir. Na kwa upande wa kampuni ya Mardev Limited mikataba ilisainiwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Omar Mouline na Shahidi wake Mwanasheria Ibrahim Jaffar.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mardev Limited, Omar Mouline amelishukuru Shirika kwa ushirikiano wote ulioipatia kampuni yake na kuahidi kufuata masharti ya mikataba hiyo.