Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar, Bi Mwanaisha Alli Said, amefanya ziara ya kikazi kwenye nyumba za Maendeleo zilizopo Makunduchi. Tukio hilo lilifanyika siku ya Jumatatu tarehe 12.07.2021 katika Tawi la  Majenzi Makunduchi.

Akiongea na Wapangaji wa Makunduchi amesema, Shirika linasikitishwa na limbukizo la deni la miaka mingi lilokueko kwa wapangaji na amewasihi kulipa deni lao ili Shirika liweze kufanya kazi zake vizuri ikiwemo kuzifanyia matengenezo nyumba hizo. 
 
Hata hivyo, aliwasisitiza Wapangaji hao kuzitunza nyumba hizo kwani sio tu maakazi yao pia Nyumba hizo ni moja ya Matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar. Na mtu yeyote atakae gundulikana anafanya matengenezo bila ya kutoa taarifa au kupata ruhusa ya Shirika atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufutwa kwa mkataba wake na kufikishwa mahakamani.

 

maku1

 

Pay to PBZ Bank


All paymets received done by Control number

Visit any ZHC Office for your Control number

Pemba Office


ZHC Branch Miembeni Chake Chake Pemba

P. O. BOX 128

Email: zhcpba@zhc.go.tz

Pemba.

Zanzibar Head Office


Zanzibar Housing Corporation

Darajani Opposite to Petrol Station

Zanzibar

P. O. BOX 795

E-mail: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Zanzibar - Tanzania