Shirika la Nyumba Zanzibar imeikodisha kampuni ya Mardev Limited yenye makaazi yake Morocco Nyumba zake nne.

mk5Shirika la Nyumba Zanzibar imeikodisha kampuni ya Mardev Limited yenye makaazi yake Morocco Nyumba zake nne, nyumba hizo zenye namba 288-289 ya Hurumzi, 291 ya Forodhani, 291B ya Forodhani pamoja na 292B ya Kiponda. Tukio hilo lilifanyika siku ya Jumatatu tarehe 07/06/2021 katika ofisi za Shirika la Nyumba Zanzibar.

Akiongea katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar, Mwanaisha Alli Said, alisema Nyumba hizo zimekodishwa kwa kampuni hiyo kwa ajili ya maakazi na wamepatiwa mkataba huo baada ya kufikia makubaliano yote pamoja na kuwalipa waliokuwa wapangaji wa nyumba hizo awali.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alisema mara tu baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo mpangaji huyo ataruhusika kutumia nyumba hizo. Pia aliwasisitiza Mardev Limited kuzitunza nyumba hizo pamoja na kufuata na kutii masharti ya mikataba hiyo

Mikataba hiyo ilisainiwa na Mkurugenzi Mkuu Bi Mwanaisha Alli na Shahidi wake Afisa Sheria Ndg. Taufik Bushir. Na kwa upande wa kampuni ya Mardev Limited mikataba ilisainiwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Omar Mouline na Shahidi wake Mwanasheria Ibrahim Jaffar.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mardev Limited, Omar Mouline amelishukuru Shirika kwa ushirikiano wote ulioipatia kampuni yake na kuahidi kufuata masharti ya mikataba hiyo.

News and Events

Ziara katika Ujenzi wa Nyumba Makaazi na Biashara Mombasa

Ziara katika Ujenzi wa Nyumba Makaazi na Biashara Mombasa

Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Zanzibar ( wa nne kushoto) ndg. Mwanaisha Ali Said akiwa katika ziara ya Waziri Ardhi...

Menejimenti ya Shirika la Nyumba na Kamati ya Baraza la Wawakilishi

Menejimenti ya Shirika la Nyumba na Kamati ya Baraza la Wawakilishi

Menejimenti ya Shirika la Nyumba wakiwa kwenye Kikao cha Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kuchunguza na kudhibiti hesabu za...

Ziara ya Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Nyumba za Maendeleo Michenzani.

Ziara ya Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Nyumba za Maendeleo Michenzani.

Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeambatana na Waziri wa Ardhi...

Ziara ya Viongozi wa ZHC na Wabunge kutoka Nchi ya Ujerumani.

Ziara ya Viongozi wa ZHC na Wabunge kutoka Nchi ya Ujerumani.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar, Bi. Mwanaisha Alli Said na menejimenti ya Shirika wameambatana na Wabunge kutoka Nchi...

Ziara ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar kukagua mradi wa matengenezo ya Nyumba namba 1699/1705 - Mnadani

Ziara ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar kukagua mradi wa matengenezo ya Nyumba namba 1699/1705 - Mnadani

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amefanya ziara ya kukagua mradi wa matengenezo ya Nyumba...

Mkutano wa Wadau kujadili fursa za Ujenzi wa Nyumba za bei nafuu Zanzibar

Mkutano wa Wadau kujadili fursa za Ujenzi wa Nyumba za bei nafuu Zanzibar

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar na Shelter Afrique kwa kushirikiana na Shirika la Nyumba Zanzibar imefanya mkutano...

Mode of Payment


All paymets received done by Control number

Paymet received though

PBZ Bank / PBZ Agent

TigoPesa / EzyPesa

Visit any ZHC Office for your Control number

Pemba Office


Mtaa wa Masingini

Barabara Kuu

P. O. BOX 349

Chake Chake Pemba

Email: zhcpba@zhc.go.tz

Zanzibar Head Office


Zanzibar Housing Corporation

Sonara Building, Darajani

Creek Road

P. O. BOX 795

E-mail: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

71124 Zanzibar..