Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar na Shelter Afrique kwa kushirikiana na Shirika la Nyumba Zanzibar imefanya mkutano wa Wadau, kwa lengo la kujifunza na kujadili fursa mbalimbali za ujenzi wa Nyumba za bei nafuu (Affordable Housing). Mkutano huo ulifanyika hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar.

Katika mkutano huo mgeni rasmi alikua Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma ambae alielezea malengo ya serikali katika kufanikisha azma hiyo ya kuwapatia Wazanzibari nyumba bora na za gharama nafuu.

Aidha, Viongozi mbali mbali wa Serikali pamoja na wadau kutoka Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi walihudhuria na kutoa michango yao na maoni juu ya kufanikisha jambo hilo.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na fursa ya Ujenzi wa Nyumba za Bei Nafuu na jinsi Serikali ilivyojipanga kutumia fursa hio katika kuleta maendeleo ya makaazi bora na salama
Zanzibar ili kukidhi mahitaji ya makaazi ya Wananchi ambayo yanaongezeka kila siku.

Pay to PBZ Bank


All paymets received done by Control number

Visit any ZHC Office for your Control number

Pemba Office


ZHC Branch Miembeni Chake Chake Pemba

P. O. BOX 128

Email: zhcpba@zhc.go.tz

Pemba.

Zanzibar Head Office


Zanzibar Housing Corporation

Darajani Opposite to Petrol Station

Zanzibar

P. O. BOX 795

E-mail: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Zanzibar - Tanzania