
Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeambatana na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Mhe. Rahma Kassim Ali na Uongozi wa Shirika la Nyumba Zanzibar katika ziara ya ukaguzi wa miundo mbinu ya maji taka ya Nyumba za Maendeleo zilizopo Michenzani. Lengo kuu la ziara hiyo ni kuangalia hali ya miundo mbinu ya nyumba hizo pamoja na kupendekeza njia mbali mbali kwa Shirika ili kuboresha miundo mbinu hayo pamoja na usafi wa nyumba hizo kiujumla. Ziara hiyo imefanyika siku ya Jumatano tarehe 17/08/2022.