
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar, Bi. Mwanaisha Alli Said na menejimenti ya Shirika wameambatana na Wabunge kutoka Nchi ya Ujerumani Mhe. Dagmar Schmidt na Mhe. Tina Rudolph pamoja na Bw. Johannes Sperrfechter katika ziara ya kutembelea nyumba za maendeleo zilizo chini ya Shirika za Kikwajuni ( Nyumba za Mjerumani). Lengo kuu la ziara hiyo ni kuangalia hali ya nyumba hizo pamoja na kupendekeza njia mbalimbali za kuziboresha.